WANENGUAJI WA TWANGA PEPETA |
Bendi
ya African Stars "Twanga Pepeta" inataraji kufanya ziara ya maonyesho
katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Mara mwishoni mwa mwezi huu wa
tatu. ziara hiyo inataraji kuanzia Mkoa wa Mwanza siku ya Ijumaa tarehe 30-03-2012.
Kesho yake siku ya Jumamosi tarehe 31-03-2012 kundi
zima la Twanga Pepeta litakuwa mkoani Mara katika ukumbi wa Musoma Club
na watamalizia ziara kwa kufanya onyesho la nguvu Wilayani Kahama Mkoa
wa Shinyanga siku ya Tarehe 01-04-2012 katika ukumbi wa Club Dimpoz.
Matayarisho
yote muhimu kwa ajili ya ziara hii yamekwisha kukamilika na Bendi
inataraji kuondoka na wanamuziki wake wote ambao wataondoka siku ya
Alhamisi alfajiri mara baada ya onyesho la Club Billicanas linalofanyika
kila siku za Jumatano.
Twanga
Pepeta wanatumia ziara hii kwa ajili ya kutambulisha albamu yao
inayotamba sasa hivi ya Dunia Daraja yenye nyimbo za'Dunia
Daraja', 'Mapenzi Hayana Kiapo', 'Kauli', 'Umenivika Umasikini', 'Mtoto
wa Mwisho' na'Penzi la Shemeji' pia watatambulisha baadhi ya wasanii
waliojiunga hivi karibuni wakiongozwa na Prince Mwinjuma Muumini Kocha
wa Dunia, Venance Geuza, Jumanne Said, Grayson Semsekwa na Mshindi wa
Shindano la 'BSS Second Chance' Hajji Ramadhani ambae anakuja rasmi kwa
ajili ya kuwapa shukrani wapenzi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa kumpigia
kura mpaka kufanikiwa
kupata ushindi wa kwanza katika shindano.
Twanga Pepeta itarudi Jijini Dar es salaam siku ya Jumatatu tarehe02-04-2012 kwa ajili ya kujitayarisha na maonyesho ya Sikukuu ya Pasaka inayotaraji kusherehekewa siku ya tarehe 08-04-2012.
Twanga
pepeta imejiandaa vilivyo ili kuwapa burudani nzuri na iliyosheheni
kila aina ya utamu kwa wapenzi watakaohudhuria maonyesho katika mikoa ya
Kanda ya Ziwa na inatoa wito kwa wapenzi kujitokeza kwa wingi ili
kujionea wenyewe ubunifu mkubwa wa kutoa burudani kwa mashabiki.
Ziara
hii ni mfululizo wa mkakati wa Twanga Pepeta wa kufanya ziara kwa ajili
ya maonyesho maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuitangaza albamu ya Dunia
daraja iliyozinduliwa Novemba mwaka jana, kabla ya kwenda mikoa ya kanda
ya Ziwa twanga pepeta imeshafanya ziara katika mikoa ya Lindi, Mtwara,
Kilimanjaro, Mbeya na Iringa na inataraji kwenda katika mikoa ya
Ruvuma, Dodoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Arusha, Tabora, Zanzibar na Kigoma hapo baadae.
Martini Sospeter
Meneja
Twanga Pepeta
Posted by : ERASTO HAPPYNESS
No comments:
Post a Comment