LAZARO NYALANDU ATEMBELEA SAUT, MWANZA
Makamu waziri wa viwanda na biashara nchini atembelea chuo cha Mtakatifu Augustine mwanza. Ziara hiyo ya siku moja ilikua kwa ajili ya kuzungumza na wanafunzi wa mwaka wa tatu kwa kozi ya Uhusiano wa Jamii na Masoko.
Mheshimiwa alizungumzia mambo mengi ila alitilia mkazo katika hoja ya UHURU.Uhuru alio uzungumzia ni katika watanzania kujielewa na kutokusubilia kila kitu kifanywe na serikali kwa maana ya viongozi wa nchi.
Alizungumzia hili akitoa mfano wa matumizi ya intanet japo kwa nchi za afrika mashariki Tanzania iliongoza tatizo ni matumizi yake.Wakati wenzetu wa Kenya wanatumia kupata mawazo ya jinsi ya kuanzisha biashara na kutangaza biashara zao Tanzania tunatumia mtandao kuwasiliana na marafiki na kutafuta udaku.
Waziri pia alieleza ni jinsi gani mitandao ya kijamii inarahisisha mawasiliano na kuchukua nafasi kubwa katika fikra za watu, hasa vijana kiasi kwamba vitu ambavyo zamani vingechukua mda mrefu kufanyiwa maamuzi sasa yanafanywa haraka kupitia mitandao hiyo. Katika kutoa changamoto waziri aliwataadharisha vijana hawa kua uoga wa kuthubutu ndio kikwazo kikubwa cha maemndeleo yao.Iwapo mitandao ya jamii imewawezesha vijana kufanya mapinduzi katika busara za maamuzi basi ni muda muwafaka mitandao hiyo ikatumika katika kukuasnya nguvu chanya katika kutambua matatizo yaliyopo nchini kwetu kwani yapo kweli na kutafuta suluhu itakayokua na tija kwa vijana na Tanzania kwa ujumla.
Swala la kujituma halikusahaulika na uhitaji wa watanzania kuacha kasumba ya kufikiria shagwe mda wote hasa wanapopata nafasi za kukutana na viongozi ila wawaze mabo ya manufaa kiuchumi kwa kutumia nafasi mda uleule nafasi zinapojitokeza.
Neno lake la mwisho lilikua ni umuhim wa wanafunzi hawa kuongeza ufaham wa mambo na kua na ujasiri ili kuondoa kasumba kua watu kutoka nchi fulani ni bora na ndio wanao kubarika zaidi.
by, mary masaga.
by, mary masaga.
No comments:
Post a Comment