VIONGOZI
wa Bunge wametakiwakuafuata majukumu yaoyakazi,
maadili na kufahamu mipaka yake ya kiutendaji ilikuepusha migogoro inayoweza kutokea.
Kauli
hiyo ilitolewal eo na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Anne Makinda wakati akifungua semina elimishi ya sikumbili ya
wajumbe waTume ya Utumishi wa Bunge na Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa
Kamati ya Uongoziwa Bunge inayoendelea katika hoteli ya White Sands
jijini Dares Salaam.
Alisema
kuwa Bunge ni mojawapo ya mihimili ya dola ni chombo muhimu katika
uongozi na hatmaya nchi yetu, hivyo umhimu wa chombo hicho nisharti
uendane na maadili ya viongozi wake.
“Ufanisi
waTaasisi ya Bunge unategemea utendaji kazi wa vyombo hivi viwili
kwasababu vyombo hivi viwili ndiyo washauri wakuu wa spika katika
kuliongoza Bunge ,” alisema SpikaMakinda.
Aliongeza
kuwa KamatiyaUongozi ndicho chombo chenye mamlaka ya kumshauri Spika
kuhusu hoja na masuala mbalimbali yatakayowasilishwa Bungeni, ambapo kwa
upande waTume ya Utumishiwa Bunge ndio kiungo kikuu cha Utawala na
Usimamizi waHuduma mbalimbali zitolewazo kwa wabunge na watumishi wa
Bunge .
Aidha
Spika Makinda aliongeza kuwa vyombo hivyo viwili vinategemeana, hivyo
ni muhimu kukutana ili kubadilishana mawazo na uzoefu wa namna ya
kutekeleza majukumu yao kwaufanisi zaidi.
Aliwataja viongozi hao kuwa wazi na huru katika majadiliano ya mada zitakazowasilishwa.
Spika
Makinda alizitaja mada zitakazowa silishwa kuwa ni tano ambazo ni
maadili, uongozi na utawala bora, majukumu yaTume ya Utumishi wa Bunge
naKamati yaUongozi na Mahusiano yake, taratibu za kiutendaji na mifumo
ya mawasiliano serikali, nafasi ya mbunge katika uongozi, itifaki na
usalama, ikiwemo mahusiano ya mihimili mitatu(Bunge, Utawala na mahakama
katika uongoziwanchi.
Naye
Mbungewa Jimbo la Kilindi, Beatrice Shellukindo alisema semina hiyo
itawasaidia kuelewa majukumu yapi yanatakiwak utekelezwa na vyombo hivyo
viwili.
POSTED by
kapinga elsie s.
No comments:
Post a Comment