Saturday, March 17, 2012

MKUTANO WA HADHALA WA CHADEMA LEO VIWANJA VYA SHULE YA MSINGI NYAMALANGO MALIMBE (SAUT)

MBUNGE WA JIMBO LA NYAMAGANA MHE. EZEKIEL WENJE AKIHUTUBIA WANANCHI ENEO LA SHULE YA MSINGI NYAMALANGO MALIMBE SAUT MWANZA.
KATIBU MKUU WA CHADEMA DK WILLBROAD SLAA AKIFUNGUA TAWI LA CHADEMA SEHEMU YA SAUT

BAADHI YA WANANCHI WAKISIKILIZA HOTUBA YA KATIBU MKUU WA CHADEMA KATIKA UWANJA WA MPIRA WA NYAMALANGO PRIMARY SCHOOL SAUT

KATIBU MKUU WA CHADEMA AKIHUTUBIA WANAFUNZI NA WANAJUMUIYA YA SAUT LEO SHULE YA NYAMALANGO ENEO LA MALIMBE SAUT



MKUTANO HUO UMEFANYIKA IKIWA NI AHADI ILIYOTOLEWA NA KATIBU MKUU WA CHADEMA KWA WANAFUNZU NA JUMUIYA YOTE YA SAUT. MZUNGUMZAJI MKUU WA LEO ALIKUWA NI MHE. DK. WILLBROD PETER SLAA AMBAPO AMESEMA SERIKARI NDIYO INAYOWEZA KUMFANYA MTU KUWA MASIKINI AU VINGINEVYO, KATIKA HOTUBA YAKE YA TAKRIBANI DAKIKA AROBAINI, DK SLAA AMEGUSIA SANA SWALA ZIMA LA UCHUMI NA MUSTAKABALI WA NCHI YETU, AMESEMA HAKUNA NCHI YOYOTE DUNIANI INAYOWEZA KUENDELEA KWA KUTEGEMA KILIMO, NJIA PEKEE YA NCHI KUENDELEA NI KUWEPO VIWANDA VYA KUZALISHA BIDHAA ZINAZOWEZA KUUZWA NJE YA NCHI, AMEONGEZA KUWA WANANCHI WANATAKIWA KUPINGA MAISHA WANAYOISHI KWA HIVI SASA KWA KUIKEMEA SERIKALI.... AWALI KABLA YA DK. SLAA KUHUTUBIA ALIKARIBISHWA NA MBUNGE WA NYAMAGANA MHE. IZEKIEL WENJE.. MKUTANO HOU UMEHUDHULIWA NA BARAZA LA MADIWANI WA CHADEMA PAMOJA NA WANAFUNZI PAMOJA NA JUMUIYA YA CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU AUGUSTINO (SAUT)

No comments:

Post a Comment