KAMPENI za lala salama za
kuwania nafasi za Ubunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) mjini hapa,
zinadaiwa kugubikwa na rushwa kwa baadhi ya wabunge wakidaiwa kupewa kati ya
Sh100,000 na Sh milioni moja.Habari zilizopatikana jana mjini hapa zinaeleza kwamba
mbunge mmoja amekabidhiwa kitita cha Sh5 milioni ili kuzigawa kwa baadhi ya
wabunge.
Baadhi ya wabunge na wagombea waliohojiwa jana, walithibitisha kuwapo kwa vitendo hivyo vya rushwa huku wakishangaa ukimya wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Naibu Msemaji wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe alisema ingawa hajafuatwa na mgombea au wakala yeyote akitaka kumhonga, vitendo hivyo ni dhahiri na havina kificho.
“Mgombea anayetoa rushwa ili achaguliwe kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki hatufai kwa sababu anaweza kuuza nchi… tuwakatae wagombea wote wa aina hii ili iwe fundisho,” alisema Zitto.
Alisema mgombea yeyote anayetoa rushwa ili kupata nafasi yoyote ile, iwe ya kisiasa au kikazi, anapoteza sifa ya kuwa kiongozi na kusisitiza kuwa wanaotoa rushwa hawawezi kuwa na uzalendo na nchi badala yake watatanguliza maslahi yao.
Mbunge mmoja wa Kanda ya Ziwa ambaye hakutaka kutajwa jina alisema suala la kampeni hizo kutawaliwa na rushwa halina ubishi.
“Mimi mwenyewe juzi alikuja mmoja wa wagombea akataka kunipa Sh300,000 nikamwuliza za nini? Akasema ananipa ni za gharama za simu nimsaidie kampeni. Lakini kesho yake akawa amenisahau akataka kunipa tena Sh200,000,” alidai.
Viwango vya rushwa vinatajwa kutofautiana kulingana na mwonekano na ushawishi alionao mbunge anayelengwa lakini vinavyotajwa ni kati ya Sh100,000 na Sh700,000
"Wabunge wengine wanapewa pia Sh200,000, wengine Sh300,000, Sh500,000 na wapo wengine wanaopewa hadi kati ya Sh700,000 na Sh milioni moja.
Wagombea wanne na ndiyo wanaotajwa zaidi kumwaga fedha hizo za rushwa. Huku ikielezwa kwamba vitendo hivyo vinafanyika kwenye hoteli walizofikia wabunge hao ambazo zimetawaliwa na pilikapilika nyingi.

POSTED By Raymond Edson
No comments:
Post a Comment