Thursday, May 31, 2012


LIBERIA'S X-LEADER CHARLES TAYLOR SENTENCED TO 50 YEARS IN JAIL...!!!

Judges at an international war crimes court have sentenced former Liberian President Charles Taylor to 50 years in prison following his landmark conviction for supporting rebels in Sierra Leone who murdered and mutilated thousands during their country's brutal civil war in return for blood diamonds.

The Special Court for Sierra Leone found Taylor guilty last month on 11 charges of aiding and abetting the rebels who went on a bloody rampage during the decade-long war that ended in 2002 with more than 50,000 dead.

Presiding Judge Richard Lussick says the crimes Taylor was convicted of were of the "utmost gravity in terms of scale and brutality."

The 64-year-old warlord-turned-president is the first former head of state convicted by an international war crimes court since the Second World War.

Taylor will serve his sentence in a British jail. His lawyers, however, are expected to appeal his convictions and that will likely keep him in a jail in The Hague, Netherlands, for months.

Prosecutors say he funnelled arms, ammunition and other supplies in return for "blood diamonds" mined using slave labour.

Presiding Judge Richard Lussick said: "The lives of many more innocent civilians in Sierra Leone were lost or destroyed as a direct result of his actions."

Taylor showed no emotion as the judge handed down what will effectively be a life sentence. Prosecutors had asked judges at the Special Court for Sierra Leone to impose an 80-year sentence; Taylor's lawyers urged judges to hand down a sentence that offered him some hope of release before he dies.Mr Lussick said an 80-year sentence would have been excessive as Taylor was convicted of aiding and abetting crimes and not direct involvement.

But the judge added that Taylor was "in a class of his own" compared to others convicted by the United Nations-backed court. "The special status of Mr. Taylor as a head of state puts him in a different category of offenders for the purpose of sentencing," Mr Lussick said.

JOYCE MWAKALUKWA

Thursday, May 24, 2012

hawa-ndio-waliojitokeza-kugombea-miss-nyamagana-2012

.
.
.
.
.
.
.
.
Watoto warembo 20 ( wengi wao wakiwa ni wanafunzi wa chuo cha Mtakatifu Agustino SAUT)wataonyesha uwezo kwenye Miss Nyamagana 2012 Gold Crest Mwanza tarehe 02/06 ambapo stage itamilikiwa na Linah, Ditto na Hafsa Kazinja alafu Mc ni mchekeshaji ambae alimaliza watu kwenye KTMA 2012 Mpoki ambapo Miss Nyamagana 2012 imeandaliwa na Stoppers Entainment ya jijini Mwanza.
 
( Joyce MWAKALUKWA )

Tuesday, April 17, 2012

Rushwa njenje ubunge wa Afrika Mashariki


KAMPENI za lala salama za kuwania nafasi za Ubunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) mjini hapa, zinadaiwa kugubikwa na rushwa kwa baadhi ya wabunge wakidaiwa kupewa kati ya Sh100,000 na Sh milioni moja.Habari zilizopatikana jana mjini hapa zinaeleza kwamba mbunge mmoja amekabidhiwa kitita cha Sh5 milioni ili kuzigawa kwa baadhi ya wabunge.

Baadhi ya wabunge na wagombea waliohojiwa jana, walithibitisha kuwapo kwa vitendo hivyo vya rushwa huku wakishangaa ukimya wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Naibu Msemaji wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe alisema ingawa hajafuatwa na mgombea au wakala yeyote akitaka kumhonga, vitendo hivyo ni dhahiri na havina kificho.

“Mgombea anayetoa rushwa ili achaguliwe kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki hatufai kwa sababu anaweza kuuza nchi… tuwakatae wagombea wote wa aina hii ili iwe fundisho,” alisema Zitto.

Alisema mgombea yeyote anayetoa rushwa ili kupata nafasi yoyote ile, iwe ya kisiasa au kikazi, anapoteza sifa ya kuwa kiongozi na kusisitiza kuwa wanaotoa rushwa hawawezi kuwa na uzalendo na nchi badala yake watatanguliza maslahi yao.

Mbunge mmoja wa Kanda ya Ziwa ambaye hakutaka kutajwa jina alisema suala la kampeni hizo kutawaliwa na rushwa halina ubishi.

“Mimi mwenyewe juzi alikuja mmoja wa wagombea akataka kunipa Sh300,000 nikamwuliza za nini? Akasema ananipa ni za gharama za simu nimsaidie kampeni. Lakini kesho yake akawa amenisahau akataka kunipa tena Sh200,000,” alidai.

Viwango vya rushwa vinatajwa kutofautiana kulingana na mwonekano na ushawishi alionao mbunge anayelengwa lakini vinavyotajwa ni kati ya Sh100,000 na Sh700,000

"Wabunge wengine wanapewa pia Sh200,000, wengine Sh300,000, Sh500,000 na wapo wengine wanaopewa hadi kati ya Sh700,000 na Sh milioni moja.

Wagombea wanne na ndiyo wanaotajwa zaidi kumwaga fedha hizo za rushwa. Huku ikielezwa kwamba vitendo hivyo vinafanyika kwenye hoteli walizofikia wabunge hao ambazo zimetawaliwa na pilikapilika nyingi.
POSTED By Raymond Edson

Sunday, April 15, 2012

BARAZA LA HABARI TANZANIA( MCT)LAKEMEA HABARI ZINAZOMHUKUMU MSICHANA LULU KUWA AMEMUUA KANUMBA




April 13, 2012 kamati ya maadili ya maadili ya baraza la habari tanzania MCT, imesikitishwa na ukiukwaji mkubwa wa maadili uliojitokeza hivi karibuni kwa baadhi ya vyombo vya habari ambavyo  wakati vikiripoti kuhusu kifo cha msanii kanumba, vimemhukumu msichana Elizabeth Michael Kimemeta maarufu kama Lulu , kuwa amemuua msanii huyo.

Ukiukwaji huo umejitokeza hasa baada ya msichana huyo kufikishwa mahakamani, ambapo baadhi ya magazeti yanayoheshimika katika jamii yaliandika vichwa vikubwa vinavyosema: LULU KORTINI KWA KUMUUA KANUMBA, NA LULU KIZIMBANI KWA MAUAJI YA KANUMBA.

Kwa mujibu wa sheria na maadili ya uandishi  habari mtu yeyote anayekamatwa kwa tuhuma yoyote ni mtuhumiwa mpaka atiwe hatiani na mahakama, Baraza pia limeshatoa matamko mara kadhaa kuwakumbusha wana habari kujiepusha na uandishi wa habari au vichwa vya habari vinavyohukumu.
Baraza linafahamu fika kuwa kesi zilizoko mahakamani ni kivutio kwa umma, kutaka kujua kinachoendelea ili kuona haki ikitendeka na pia wanahabari wana haki ya kujua na kuripoti yanayojiri huko na katika vyombo vingine vya sheria.

Ni wazi kuwa vichwa vya habari vilivyotajwa hapo juu vimeingilia uhuru wa mahakama kwa kuchapisha habari ambazo zinaonekana kushawishi na kushinikiza uamuzi wa mahakama.
Baraza la habari linawakumbusha wahariri kuhakikisha kuwa wanafanya kazi yao kwa kuzingatia maadili, na weledi katika kuripoti mkasa huu unaogusa hisia za watu.

                                                                     Imetolewa na jaji 
Thomas B. Mihayo
 Mwenyekiti, kamati ya maadili ya baraza la habari Tanzania



POSTED BY MADUHU SALOME



Friday, March 30, 2012

Tibaigana kuihukumu Yanga leo

KAMATI ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF chini ya Mwenyekiti  Alfred Tibaigana, leo inategemewa kutoa hukumu ya wachezaji wa Yanga waliomshambulia mwamuzi Israel Nkongo kwenye mchezo dhidi ya Azam.

Kamati hiyo wiki iliyopita iliwashangaza wengi baada ya kusimamisha adhabu kwa wachezaji  wa Yanga kwa madai Kamati ya Ligi iliyotoa adhabu ya kuwafungia wachezaji hao haikuwa na mamlaka ya kufanya hivyo.

Akizungumza jijini jana, Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kamati ya Tibaigana ilikutana jana jioni mara baada ya kuwasilishwa kwa rufani ya Yanga na kusikilizwa hivyo maamuzi juu ya wachezaji hao itatolewa leo.

Alisema mara baada ya Kamati ya Nidhamu kusimamisha adhabu za wachezaji hao walipewa muda wa wiki mbili kuhakikisha wanawasilisha maamuzi ya Kamati yaLigi pamoja na rufaa iliyokatwa na Yanga kupinga adhabu hiyo.

"Kikao cha Kamati ya Nidhamu kinakutana leo jioni (jana)baada ya kukamilisha utaratibu wote ikiwemo kupeleka rufaa ya Yanga waliyokata kupinga adhabu yao pamoja na maamuzi ya kamati ya ligi iliyowafungia wachezaji wa Yanga mara baada ya kikao hicho maamuzi ya mwisho juu ya wachezaji hao itatolewa," alisema Wambura.

Wachezaji wa Yanga waliofungiwa na hatimaye kufunguliwa kwa muda ni Stephano Mwasika (mwaka moja), Jerryson Tegete (miezi sita), Nadir Haroub (mechi sita), Omega Seme na Nurdin Bakari walifungiwa kila moja mechi tatu na wote walitakiwa kulipa fidia kwa kitendo chao hicho cha kumshambulia mwamuzi.

Wakati huo huo; Mabingwa hao watetezi, Yanga tayari wamewasili jijini Tanga kujiandaa na mchezo wao wa kesho wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Akizungumza na gazeti hili, Katibu Mkuu wa Yanga, Selestine Mwesigwa alisema kikosi hicho kimeondoka Dar es Salaam na wachezaji wote pamoja na wale waliokuwa wamefungiwa na kufunguliwa.

Mwesigwa alisema Kamati ya Tibaigana ni kamati huru hivyo hakuna sababu ya kuwaacha au kuogopa kuwachezesha wachezaji waliofungiwa kwa kuwa adhabu yao imesimamishwa kwa muda wa siku 14 ambazo bado hazijakwisha.

Naye kocha Kostadin Papic alisema kikosi chake kipo imara kwa ajili ya mchezo huo huku akiwe wazi kuhusu suala la kuwatumia nyota wake wanaosubiri hukumu leo.

Papic alisema ikibidi watacheza ingawa hafikirii kama watacheza kwa kiwango chao kwa kuwa walishakata tamaa ya kucheza hivi karibuni.

"Kwenye mazoezi wamefanya vizuri baada ya kufunguliwa kwa muda, lakini siamini kama watacheza kwa ari kwa kuwa walishakata tamaa, ila ikibidi kuwatumia nitawatumia,"alisema Papic.

Posted by Raymond Edson

Waziri matatani Arumeru - VIJANA WA CHADEMA WAMZINGIRA , AHOJIWA NA POLISI

VIJANA WA CHADEMA WAMZINGIRA , AHOJIWA NA POLISI

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodlucky Ole Medeye juzi usiku aliingia matatani baada ya kutiwa msukosuko na vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakimtuhumu kujihusisha na utoaji rushwa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge zinazoendelea Jimbo la Arumeru Mashariki.

Tukio hilo, lilitokea kati ya saa 12:30 jioni na saa 1.20 usiku eneo la Kata ya Mbuguni wilayani Arumeru, pale Naibu Waziri huyo alipokurupushwa na vijana hao, kisha kukimbilia Shule ya Msingi Oldevesi, kabla ya kuokolewa na polisi.

Taarifa kwamba Medeye amekamatwa, zilisambaa kwa kasi hali iliyosababisha watu kadhaa kwenda Kituo cha Polisi Usa River kupata taarifa kamili za tukio hilo, lakini ilifahamika kuwa, Naibu waziri huyo hakufikishwa polisi baada ya kutolewa Mbuguni.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye akizungumza na Mwananchi kwa simu jana, alisema walipata taarifa kutoka kwa vijana hao juzi kwamba Naibu Waziri huyo alikuwa anafanya kampeni eneo la Shambarai.

Gazeti hili lilipomtafuta Naibu waziri huyo kupata ukweli wa tukio hilo,  alikiri kukumbwa na mkasa huo, lakini alikanusha madai kwamba alikuwa akigawa fedha kwa lengo la kukisaidia Chama Cha Mapinduzi(CCM).

Hata hivyo, habari kutoka Mbuguni zilizolifikia Mwananchi, zilidai kuwa Medeye ambaye pia ni Mbunge wa Arumeru Magharibi, alikutwa na mkasa huo alipokuwa kwenye mazungumzo na mmoja wa wamiliki wa mashamba makubwa katika eneo hilo, mwenye asili ya kiasia (jina tunalihifadhi), pamoja na wanawake kadhaa ambao ni wakazi wa kata hiyo.

Baadhi ya vijana wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chadema, walimzingira Medeye na kuanza kumhoji sababu za kuwepo eneo hilo  na kugawa fedha kwa lengo la kukisaidia CCM huku akitumia gari la Serikali, hali iliyozua tafrani na kusababisha Naibu Waziri huyo kutimua mbio hadi Shule ya Msingi Oldeves.

Wakati wakiendelea kujibizana, mmoja wa vijana hao alimpiga picha Naibu Waziri huyo pamoja na gari hilo lililokuwa na bendera ya taifa, na kwamba kitendo hicho kilimkera kiongozi huyo kiasi cha kutaka kuvunja kamera, hatua iliyochangia kuongeza kwa tafrani hiyo.

“Baada ya hali ya hewa kuchafuka, baadhi ya wakereketwa wa CCM walipiga simu Kituo cha Polisi Mbuguni, askari wakafika mara moja na kuondoka na Medeye hadi Kituo cha Polisi Mbuguni," alidai mmoja kati ya mashuhuda wa tukio hilo.

Ilikuwaje?

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema,  Zanzibar,  Hamid Mussa Yusuph, ambaye alikuwa eneo la tukio, alisema wakiwa katika kazi ya kutangaza mikutano ya chama chao juzi, waliona gari la waziri huyo na walipolisogelea, walimkuta akiwa jirani huku akizungumza na  mkulima huyo mwenye asili na kiasia na baadhi ya akina mama.

"Sisi tulimhoji anafanya nini jioni katika eneo hilo akiwa na gari la Serikali? Akatujibu ana shughuli zake, hapo yakatokea majibizano, ndipo alikimbia kwenda kujihifadhi Shule la Oldevesi," alisema Yusuph.

Alisema kutokana na idadi ya watu kuendelea kuongezeka katika eneo hilo, yeye (Yusuph) aliamua kupiga simu polisi, kuwaarifu na kwamba baada ya muda mfupi, askari walifika na baada ya kumhoji sababu za yeye kuwepo hapo, waliondoka naye.

Yusuph alisema baada ya hapo, waliamua kwenda kutoa taarifa polisi na kufungua faili la uchunguzi ambalo lilipewa namba MNG/RB/81/2012 na baadhi ya wanachama waliokuwepo, waliandika maelezo yao.

Hata hivyo jana Mkuu wa Operesheni wa Polisi katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, Naibu Kamishna, Isaya Mngulu, alisema hakuna jalada lolote lililofunguliwa kuhusu tukio hilo na wala polisi hawajamshikilia Naibu Waziri huyo.

Baada ya Mngulu kutajiwa namba ya faili la keshi iliyofunguliwa Mbuguni, alisema: “Mimi sina hiyo taarifa bwana, labda kama ndio hivyo mtafute RCO (Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Arusha) akueleze zaidi”.

Aliongeza: "Ninachojua mimi hakuna kesi yoyote ya Naibu Waziri huyo na kama kuna faili limefunguliwa, atafutwe huyo Mkuu wa Upelelezi".
POSTED by: MASEBO FlORA, J

Monday, March 26, 2012

Twanga Kufanya Ziara ya Nguvu Mwanza, Shinyanga na Mara

WANENGUAJI WA TWANGA PEPETA
Bendi ya African Stars "Twanga Pepeta" inataraji kufanya ziara ya maonyesho katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Mara mwishoni mwa mwezi huu wa tatu. ziara hiyo inataraji kuanzia Mkoa wa Mwanza siku ya Ijumaa tarehe 30-03-2012.

Kesho yake siku ya Jumamosi tarehe 31-03-2012 kundi zima la Twanga Pepeta litakuwa mkoani Mara katika ukumbi wa Musoma Club na watamalizia ziara kwa kufanya onyesho la nguvu  Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga siku ya Tarehe 01-04-2012 katika ukumbi wa Club Dimpoz.

Matayarisho yote muhimu kwa ajili ya ziara hii yamekwisha kukamilika na Bendi inataraji kuondoka na wanamuziki wake wote ambao wataondoka siku ya Alhamisi alfajiri mara baada ya onyesho la Club Billicanas linalofanyika kila siku za Jumatano.
Twanga Pepeta wanatumia ziara hii kwa ajili ya kutambulisha albamu yao inayotamba sasa hivi ya Dunia Daraja yenye nyimbo za'Dunia Daraja', 'Mapenzi Hayana Kiapo', 'Kauli', 'Umenivika Umasikini', 'Mtoto wa Mwisho' na'Penzi la Shemeji' pia watatambulisha baadhi ya wasanii waliojiunga hivi karibuni wakiongozwa na Prince Mwinjuma Muumini Kocha wa Dunia, Venance Geuza, Jumanne Said, Grayson Semsekwa na Mshindi wa Shindano la 'BSS Second Chance' Hajji Ramadhani ambae anakuja rasmi kwa ajili ya kuwapa shukrani wapenzi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa kumpigia kura mpaka kufanikiwa
kupata ushindi wa kwanza katika shindano.

Twanga Pepeta itarudi Jijini Dar es salaam siku ya Jumatatu tarehe02-04-2012 kwa ajili ya kujitayarisha na maonyesho ya  Sikukuu ya Pasaka inayotaraji kusherehekewa siku ya tarehe 08-04-2012.

Twanga pepeta imejiandaa vilivyo ili kuwapa burudani nzuri na iliyosheheni kila aina ya utamu kwa wapenzi watakaohudhuria maonyesho katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na inatoa wito kwa wapenzi kujitokeza kwa wingi ili kujionea wenyewe ubunifu mkubwa wa kutoa burudani kwa mashabiki.

Ziara hii ni mfululizo wa mkakati wa Twanga Pepeta wa kufanya ziara kwa ajili ya maonyesho maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuitangaza albamu ya Dunia daraja iliyozinduliwa Novemba mwaka jana, kabla ya kwenda mikoa ya kanda ya Ziwa twanga pepeta imeshafanya ziara katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Kilimanjaro, Mbeya na Iringa na inataraji kwenda katika mikoa ya
Ruvuma, Dodoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Arusha, Tabora, Zanzibar na Kigoma hapo baadae. 

Martini Sospeter
Meneja 
Twanga Pepeta
Posted by : ERASTO HAPPYNESS